ZEC inamuhujumu Rais Hussein Mwinyi kwa makusudi – Duni

Makamu Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo upande wa Zanzibar, Juma Duni Haji, anasema ana uhakika sasa kwamba Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) inamuhujumu kwa makusudi Rais Hussein Ali Mwinyi kwa jinsi inavyomuharibia heshima yake kwenye suala la Maridhiano na Umoja wa Kitaifa. Hii ni kufuatia jinsi ilivyoendesha na kusimamia chaguzi ndogo za uwakilishi jimbo la Pandani kisiwani Pemba na udiwani wadi ya Kinuni kisiwani Unguja leo.

Post Author: CoinCryptoNews