Serikali yatoa kauli kuhusu ada elekezi kwa shule binafsi, yapanga kuunda ‘Bodi ya Walimu’

Serikali yatoa kauli kuhusu ada elekezi kwa shule binafsi, yapanga kuunda ‘Bodi ya Walimu’

Serikali imesema haina mpango wa kuweka ada elekezi kwa shule binafsi, bali itajikita zaidi kwenye kuboresha kiwango cha elimu.

Naibu Waziri wa Elimu William Olenasha ndiye aliyetoa kauli hiyo bungeni leo wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Mariam Kisangi.

Olenasha pia amesema serikali iko mbioni kuunda Bodi ya Walimu ambayo itahusika pia kusimamia viwango vya walimu wanaoajiriwa kwenye shule binafsi.

Related Post: